Robert Kyagulanyi ambaye anajulikana pia kwa jina lake la usanii Bobi Wine, amekuwa mwiba kwa uongozi wa rais Museveni, akivutia maelfu yawaganda kote aliko fanya kampeni zake zakuwania urais.
Hata hivyo, baadhi ya wachambuzi wanahisi ni mapema sana kwa Bobi Wine kuwa rais wa taifa hilo la mashariki ya Afrika, na kwamba rais Museveni angali na uvutio wakutosha miongoni mwa wapiga kura wengi nje ya mji mkuu wa Kampala.
Idhaa ya Kiswahili ya SBS ilizungumza na Bw William ambaye ni mzawa wa Uganda, kuhusu kampeni za urais za mwaka huu, pamoja na mtazamo wake kwa yale ambayo waganda watazingatia wanapo ingia katika vyumba vyakupiga kura.

Mgombea wa urais wa Uganda Robert Kyagulanyi, anayejulikana pia kama Bobi Wine, azungumza na mashabiki katika mji wavibanda wa Kibera jijini Nairobi. Source: AFP

Yoweri Museveni awasalimia wafuasi wake katika uwanja wandege wa Kololo Kampala, Uganda 2016. Source: AP
Bofya hapo juu kwa taaifa kamili.