Janga la COVID-19 lime waongezea wajasiriamali shinikizo na changamoto za ziada, wengi wao wakiachwa na uamuzi mgumu kuhusu hatma za biashara na uwekezaji wao.
Bw Freddy ni mjasiriamali ambaye huwekeza katika biashara za migahawa jijini Brisbane, katika mazungumzo maalum na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, alifunguka kuhusu changamoto ambazo janga la COVID-19 lime zua na baadhi ya maamuzi magumu ambayo yeye pamoja na wajasiriamali wenza wana kabiliana nayo.