Wengi wamesema kutangazwa kwa mipango yakuanzishwa kwa ligi kuu maalum barani ulaya, ambayo itajumuisha baadhi ya timu zitakazo shiriki kwa mwaliko maalum, ilikuwa hatua ya mwisho ambayo mashabiki wengi hawakuweza vumilia.
Tangazo hilo lilizua gumzo kote duniani na mashabiki wengi wa soka nchini Uingereza, waliandamana mbele ya viwanja vya mpira vya vilabu vyao, ila mashabiki wa Manchester United walichukua hatua ya ziada nakuingia hadi ndani ya uwanja wao nakusababisha mechi kati ya watani wao wa jandi Liverpool kuahirishwa kwa misingi ya usalama.
George ni mmoja wa mashabiki wakubwa wa Manchester United wanao ishi nchini Australia, aliweka wazi baadhi ya kero na sababu za mashabiki wenza kuandamana dhidi ya mmiliki wa timu yao, pamoja na matarajio yake kwa matokeo ya maandamano hayo. Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.