Watch FIFA World Cup 2026™

LIVE, FREE and EXCLUSIVE

Australia Yafafanuliwa:Je, mashirika ya kutoa misaada na watu wanao changisha hela hufanyaje kazi nchini Australia?

BlurGettyImages-1075808762.jpg

募款人员必须清楚说明慈善机构的性质和职责。 图片来源:Scott Barbour / Cricket Australia via Getty Images

Je, ni sheria gani zinazo husu kuchangisha pesa na mashirika ya kutoa misaada? Unawezaje hakikisha kuwa hutadanganywa? Haya ndiyo unastahili jua kama una toa mchango, unachangisha pesa mwenyewe au una zindua ombi la mchango mtandaoni.


Published

Updated

By Zoe Thomaidou

Presented by Gode Migerano

Source: SBS



Share this with family and friends


Je, ni sheria gani zinazo husu kuchangisha pesa na mashirika ya kutoa misaada? Unawezaje hakikisha kuwa hutadanganywa? Haya ndiyo unastahili jua kama una toa mchango, unachangisha pesa mwenyewe au una zindua ombi la mchango mtandaoni.


Key Points

  • Rules on how fundraisers are conducted differ across Australian jurisdictions.
  • To avoid fundraising scams, take the time to check a charity’s credentials and refrain from donating if in doubt.
  • Fundraising laws and licence requirements also apply to small fundraisers and online appeals, so you should check what applies in your case.

Sikiliza makala yetu yaliyo rekodiwa hapa

Sekta ya hisani ya Australia imeundwa na mashirika ya hisani yenye ukubwa tofauti, kuanzia vikundi vya jamii vya ndani hadi mashirika ya misaada ya kimataifa.

Siyo mashirika yote madogo ya hisani yamesajiliwa na mdhibiti wa kitaifa, Tume ya Hisani ya Australia na Mashirika Yasiyo ya Faida (ACNC).

Naweza tazama vipi kama shirika la hisani ni halali?

Ni rahisi kuangalia sifa za shirika la hisani kama liko kwenye sajili ya hisani ya ACNC.

Kuwa katika sajili ya ACNC inamaanisha shirika la hisani limepimwa ili kufikia vigezo fulani, kama vile hali isiyo ya faida na kufuata viwango vya utawala.

Unashauriwa kuangalia kwenye sajili kabla yakutoa mchango, Kamishna wa ACNC Sue Woodward anasema.

"Kwa sababu inaweza kupa taarifa kuhusu nani anayeendesha shirika hilo la hisani, aina ya shughuli linazofanya, wapi linapata pesa zake.

"Na pia unaweza pata imani kwamba ni shirika halisi la hisani lililosajiliwa na wana wajibu wa kufuata sheria fulani kuhusu utawala bora."

Je, mchango wangu unaweza punguziwa kodi?

Unaweza dai makato ya kodi pekee kwa michango inayotolewa kwa mashirika ya kutoa misaada yaliyoidhinishwa na Ofisi ya Ushuru ya Australia ili iwe na hadhi ya Mpokeaji wa Zawadi Anayeweza punguzwa.

Tembelea ABN Lookup kutazama kama shirika la msaada lina hadhi ya DGR.

Weka risiti kama kumbukumbu ya mchango wako kama unapanga kudai punguzo la kodi.

Australia Explained - Fundraising
Not all registered charities can issue tax deductible receipts for donations. Credit: FujiCraft/Getty Images

Nani anadhibiti michango ya fedha?

Kila jimbo na wilaya nchini Australia ina sheria zake za kuchangisha fedha na mamlaka za udhibiti.

“ACNC si mdhibiti wa uchangishaji wa fedha,” Kamishna Woodward anasema.

"Kwa mfano, kama shirika linakusanya pesa kutoka kwa umma katika kituo cha ununuzi, kuna sheria maalum ambazo watalazimika kufuata ambazo hutofautiana kulingana na jimbo uliko."

Wachangishaji wa fedha wanaweza pia kuidhinishwa na serikali za mitaa na sheria zingine, kama vile Sheria ya Mtumiaji ya Australia and sheria za Faragha.

Kama una wasiwasi kuhusu mwenendo wa shirika la hisani wa kuchangisha fedha, unaweza wasilisha wasiwasi huo kwa mdhibiti wa jimbo au wilaya yako.

Kwa muhtasari wa sheria za kuchangisha fedha na taarifa kuhusu mdhibiti wa eneo unako ishi, bofya viungo vilivyo hapa chini:

Kama unaamini shirika la kutoa misaada lililosajiliwa halisimamii fedha ipasavyo, unaweza liripoti kwa ACNC. 

"Wakitaka, wanaweza fanya hivyo bila kujitambulisha na tunachukulia masuala hayo kwa uzito," Kamishna Woodward anasema.

Australia Explained - Fundraising
Be on the lookout for fake appeals, especially following a disaster or tragic event. Credit: bymuratdeniz/Getty Images

Nitajuaje kama uchangishaji pesa fulani ni ulaghai?

Kuepuka ulaghai wa uchangishaji pesa mtandaoni, tazama kama uko kwenye tovuti rasmi nakuwa mchango huo ni halali

Kama una shaka kuhusu kuchangisha fedha ana kwa ana, usitoe mchango, Peter Hills-Jones anasema.

Yeye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Udhibiti wa Uchangishaji Fedha cha Umma, shirika la tasnia linalowakilisha mashirika ya hisani na mashirika ya kuchangisha fedha yanayofanya uchangishaji fedha ana kwa ana nchini Australia.

Usiwe na haraka, tulia... daima unaweza enda kwenye tovuti au kupigia simu shirika hilo la misaada kisha unaweza toa mchango baadae.
Peter Hills-Jones

Bw. Hills-Jones anaelezea maswala matatu hatari ambayo yanaweza kuonyesha ulaghai wa kuchangisha fedha ana kwa ana.

  • Mtu binafsi anaye changisha fedha hajavaa sare.
  • Hawana kitambulisho chenye picha yake 
  • Wanaomba mchango wa pesa taslimu au wa mara moja 
Fundraising at football
Face-to-face fundraisers are mandated to behave with professionalism and respect. Credit: James Wiltshire/AFL Photos via Getty Images

Wachangishaji fedha ana kwa ana wameamriwa kufanya kazi kwa weledi na heshima, kwa mfano kutowazuia watu wakiwa nje au kuwakaribia walipoketi.

"Wachangishaji fedha wanahitaji elezea wazi jukumu la shirika la hisani, kwa nini wanaomba pesa.

"Na kama mtu binafsi mtaani au mlango kwa mlango hajisikii kama anataka kutoa mchango, matakwa yake yanapaswa heshimiwa."

Ukishuku ulaghai wa kuchangisha pesa, kataa kutoa mchango na uripoti kwa mdhibiti wa eneo lako au huduma yakitaifa ya Ulaghai.

Nastahili jua nini kama na changishia swala fulani hela?

Watu wanaochangisha pesa wanapaswa kumbuka kwamba kile kinachohesabiwa kama ufadhili unaodhibitiwa hutofautiana katika majimbo na wilaya.

Mwanasheria Amy Williams, kutoka shirika la Justice Connect’s shirika lisilo la faida la huduma ya sheria, anashauri daima kuuliza mdhibiti wako wa michango aangalie sheria gani unastahili fuata.

Isipokuwa kama unatoa ombi la kibinafsi la pesa.

"Mambo kama kuwaomba marafiki au familia yako pesa ili kusaidia tukio la kujitolea nje ya nchi au kuchangisha pesa kazini ikiwa una mfanyakazi anayehitaji kulipiwa gharama za matibabu, maswala haya kwa kawaida hayadhibitiwi na sheria za kuchangisha pesa," Bi. Williams anaelezea.

Australia Explained - Fundraising
There are three main types of face-to-face fundraisers: street, door-to-door and fundraisers operating within shopping centres. Credit: LeoPatrizi/Getty Images

Sheria za kuchangisha hela mtandaoni ni gani?

Ukizindua ombi la kuchangisha fedha mtandaoni, kwa mfano kupitia jukwaa la kuchangisha fedha kwa watu wengi, Bi. Williams anasema kuna uwezekano mkubwa unahitaji kufuata sheria za kuchangisha fedha katika mamlaka nyingi.

Kama unachangisha fedha mtandaoni kwa jukwaa la watu wengi, unaweza hitaji leseni katika kila jimbo na wilaya.
Amy Williams

"Baadhi ya majukwaa ya kuchangisha fedha yatakupa mwongozo, wakati mwingine hayaeleweki vizuri kuhusu hilo na unahitaji kutafuta ushauri wako wa kisheria."

Hatimaye, anasema, michango ya mtandaoni inapaswa kufafanua wazi sababu iliyokusudiwa ya pesa zilizokusanywa, ili kuepuka kuwapotosha wafadhili.

"Wafadhili pia wanapaswa kuuliza swali 'Je, madhumuni ya shirika hili ni nini?' Ili uweze kuelewa fedha zitaenda wapi."

Jisajili au fuata podikasti ya Australia Yafafanuliwa kwa taarifa na vidokezo muhimu zaidi kuhusu kuanza maisha yako mapya nchini Australia.

Je una maswali au mawazo ya mada? Tuma barua pepe australiaexplained@sbs.com.au


Latest podcast episodes

Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Stream now