Wakaazi wa mji wa Goma pamoja na mamlaka husika wanaendelea kuwatafuta wahanga pamoja naku tathmini uharibifu ulio sababishwa na mlipuko wa volcano hiyo.
Ila, watu wengi wanahoji kwanini shirika la Goma Volcano Observatory, ambalo linajukumu lakuchunguza nakufuatilia maswala ya volcano katika eneo hilo kwa nini haliku waonya wakaazi kuhusu uwezekano wa mlipuko wa volcano hiyo.
Blaise ni kiongozi wa zamani wa jamii yawatu kutoka Jamuhuri yakidemokrasia ya Congo, wanao ishi mjini Sydney, Australia. Katika mazungumzo maalum na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, aliweka wazi baadhi ya sababu ambazo watu wengi wanaishi katika eneo hilo lenye hatari ya mlipuko wa volcano.