Kujibu changamoto hiyo, shirika la Nakango Vision Inc lenye makao makuu katika kitongoji cha Fairfield, New South Wales, Australia lime fungua shule yakiswahili na kifaransa.
Kila Jumamosi asubuhi, wavulana kwa wasichana wenye umri tofauti, hufunzwa Kiswahili na Kifaransa katika darasa hilo.
Idhaa ya Kiswahili ya SBS ilitembelea shule hiyo, nakuzungumza na mwalimu pamoja na baadhi ya wanafunzi walio weka wazi hisia zao kuhusu kufundisha nakufunzwa Kiswahili katika shule hiyo. Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.