Shirika la Great Lakes Agency for Peace and Development International (GLAPD) kwa ushirikiano na chuo cha Western Sydney, lili fanya utafiti kwa swala la unyanyasaji wa nyumbani naku zindua ripoti hiyo hivi karibuni.
Rosemary Kariuki ni mshindi wa tuzo ya shujaa wa jamii nchini Australia, alihudhuria uzinduzi huo ambapo alichangia maoni yake na Idhaa ya Kiswahili kuhusu ripoti hiyo pamoja naku fafanua baadhi ya dalili na ishara za unyanyasaji wa nyumbani.