Wakati mvua kali ime endelea kusababisha mitandao ya mito kufurika, baadhi yajamii katika maeneo ambayo huathiriwa kwa mafuriko, yameshuhudia uharibifu mkubwa kwa miundombinu, nyumba na hata kupoteza maisha.
Kwa hiyo utajuaje kama tukio kubwa la hali ya hewa linakaribia na, unastahili fanya nini kujitayarisha? Unaweza omba nani msaada na je, unastahili baki ama ondoka unako ishi?
Ni mhimu pia kutazama kama sera ya bima yako bado iko sawa na kama inatosha. Hakikisha inakufunika kwa kila aina yamatukio yanayo husiana na unako ishi.
Matukio hayo yanaweza jumuisha mafuriko ya ghafla, mtiririko wa maji ya dhoruba, mimonyoko ya ardhi pamoja na uharibifu unao sababishwa na miti au vitu vinavyo anguka.