Jinsi yakupata msaada wakisheria bure Australia

Mwanasheria amhudumia mteja

Mwanasheria amhudumia mteja Source: Getty Images

Mfumo wa sheria wa Australia unaweza wachanganya watu wa kawaida na, msaada wakitaalam unaweza hitajika kuukabili.


Ila wakati huduma ya wanasheria inagharimu maelfu ya dola kwa saa, sikila mtu anaweza mudu kufuatilia haki yake. Hata hivyo, unaweza weza pata msaada kupitia shirika la legal aid bila malipo yoyote. Profesa wa Sheria Dr Jeff Giddings kutoka chuo cha Monash, anasimamia mradi wa msaada wa sheria ya familia, mradi huo ume undwa kuwasaidia watu wanao jiwakilisha katika kesi za sheria ya familia.

Shule zingine za sheria nchini Australia zinazo toa msaada zinajumuisha vyuo vya Griffith, Deakin, Bond na vyuo vingine. Katika vituo vya sheria, wanafunzi hutoa msaada na taarifa kuhusu mchakato wa sheria na jinsi mahakama hutumika bure, chini ya usimamizi wa wakili mzoefu. Kuna aina tofauti pia ya tovuti zinazo toa taarifa yakisheria bure, kukusaidia kukabiliana na mfumo wa mahakama. Kesi yakisheria ya Maria, inayo husu malezi ya watoto wake inaendelea.

Hakutimiza masharti ya vipimo vya uwezo vya shirika la Legal Aid, kwa sababu anachangia katika umiliki wa nyumba na alipewa orodha ya mawakili wanao toa huduma bure. Licha ya miaka kupitia na kuwasiliana na mawakili wengi katika orodha hiyo, bado anatafuta mtu atakaye simamia kesi yake bure. Kwa taarifa zaidi kuhusu huduma za bure zakisheria katika jimbo au wilaya yako, tembelea tovuti ya Australian Pro Bono Centre. www.probonocentre.org.au


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service