Bi Bishop amesema hatawania kiti chake cha ubunge cha Curtin jimboni Magharibi Australia, katika uchaguzi mkuu ujao.
Bi Bishop amesema ana amini serikali ya mseto ita shinda uchaguzi mkuu wa shirikisho bila msaada wake.
Ameongezea kuwa atafanya kazi kwa bidii, kuhakikisha mgombea wa chama cha Liberal anashinda uchaguzi wakugombea eneo bunge lake la zamani.





