Julie Bishop ni shahidi wa "tabia mbovu" za wabunge

Julie Bishop azungumzia dhulma katika bunge la taifa

Julie Bishop amesema ameshuhudia tabia mjini Canberra, ambayo haiwezi vumiliwa katika sehemu zingine za kazi nchini Australia. Source: AAP

Mmoja wa wabunge maarufu wa serikali, amekosoa unyanyasaji ndani ya chama chake.


Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Australia Julie Bishop, amesema tabia ambayo ame shuhudia Canberra haiwezi kubaliwa mahali pengine.

Licha ya ukosoaji huo baadhi ya wanachama wa Liberal, wame sema hawaja ona ushahidi wowote. Baadhi ya watu weme dokeza kuna unafiki kwa upande wa Bi Bishop.

Waziri Mkuu wa zamani Julia Gillard alipo toa hotuba yake maarufu kuhusu chuki dhidi ya wanawake mjini Canberra, Bi Bishop alisema waziri mkuu wa zamani alikuwa akijifanya mwathirika.

Kwa upande wake waziri mkuu Scott Morrison, amedokeza kuwa atakabiliana na swala hilo.

Ila wakati kuna baadhi ya wanachama ambao wako tayari kutaja majina naku aibisha wanyanyasaji ndani ya chama tawala, na uhuru mpya ambao Julie Bishop amepata baada yakuvuliwa majukumu ya uwaziri, hali hiyo huenda ikawa tatizo sugu kwa kiongozi mpya wa chama tawala.


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service
Julie Bishop ni shahidi wa "tabia mbovu" za wabunge | SBS Swahili