Wanachama wa jumuiya yawa Afrika wanao ishi Canberra, ACT wanajiandaa kushiriki katika kombe la Afrika kesho Jumamosi 14 Septemba 2024.
Michuano hiyo ya kila mwaka huwaleta wanajumuia pamoja, kuchangia uzoefu na utamaduni wao kupitia soka, muziki na vyakula. Timu za wanaume na wanawake hushiriki katika michuano hiyo.

Bw Kinyua ni mmoja wa waandalizi wa michuano hiyo, katika mazungumzo maalum na SBS Swahili alifunguka zaidi kuhusu malengo na faida ya michuano hiyo.
Bonyeza hapo juu kwa mahojiano kamili.
Share





