Katika ziara zake nyingi alisimama nakusikiza kero zao, nyingi ambazo alitatua papo hapo na zingine aliacha maagizo zifanyiwe kazi. Miongoni mwa walio wasilisha kero zao ni wajasiriamali wengi ambao, mara kwa mara walikabiliana na masharti magumu kutoka kwa mamlaka.
Louis Amon ni mjasiriamali nchini Australia mwenye asili ya Tanzania, alizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya SBS nakuweka wazi hisia za wajasiriamali wakitanzania, na pigo ambalo wamepata kupitia kifo cha kipenzi chao.
Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.