Mlipuko wa volcano hiyo ulitokea bila onyo lolote, na ulisababisha vifo vya watu 15 pamoja na uharibifu wa zaidi ya nyumba 500 pamoja na mali nyingi sana.
Mama Elie ni mkaazi wa jimbo la Victoria, Australia. Katika mazungumzo maalum na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, alitueleza jinsi wanachama wa familia yake walijinusuru kutoka mlipuko wa volcano hiyo pamoja na uharibifu na hasara iliyo sababishwa.