Jamii yawakenya wanao ishi mjini Sydney, NSW, Australia, katika siku chache zilizo pita wamekuwa wakifika viwanjani kwa kishindo.
Sababu yao kufika viwanjani ilikuwa kuwapa moyo timu yao, iliyokuwa ikishiriki katika kombe la Afrika, baada ya miaka mingi kuwa jangwani.
Punde baada ya mechi ya mwisho yakundi A, mashabiki hao walichangia maoni yao kuhusu timu yao na Idhaa ya Kiswahili ya SBS.
Share






