Mh Dkt Luc Mulimbalimba, ni mbunge katika Jamuhuri yakidemokrasia ya Kongo pamoja nakuwa daktari wa binadam na mwanzilishi wa hospitali katika jimbo la Kusini Kivu.
Hospitali hiyo huwa hudumia wakazi wamaeneo ya jimbo hilo, pamoja na wakazi kutoka nchi jirani kama Burundi. Alipotembelea studio za Radio ya SBS, Mh Dkt Mulimbalimba aliweka wazi hatua ambazo serikali ya Jamuhuri yakidemokrasia ya Kongo, imechukua kukabiliana na janga hili la coronavirus pamoja na hatua ambazo amechukua yeye binafsi kama daktari, kutoa taarifa na huduma kwa wakaazi wa eneo bunge lake.
Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.