Watch FIFA World Cup 2026™

LIVE, FREE and EXCLUSIVE starting June 12 2026

MiniPod: GOAT | Words we use

WWU_S2_EP1_GOAT.png

G.O.A.T. is short for Greatest Of All Time, but there is more behind it.

Jifunze msemo mpya na fanya Kiingereza chako kisikike cha asili na cha kuvutia zaidi. Words we Use ni makala ya lugha mbili, yatakayo kusaidia kuelewa nahau kama vile 'G.O.A.T' (Mchezaji Bora wa Wakati Wote).


Published

By Nick Pagano

Presented by Gode Migerano

Source: SBS



Share this with family and friends


Jifunze msemo mpya na fanya Kiingereza chako kisikike cha asili na cha kuvutia zaidi. Words we Use ni makala ya lugha mbili, yatakayo kusaidia kuelewa nahau kama vile 'G.O.A.T' (Mchezaji Bora wa Wakati Wote).


GOAT- labda umewahi sikia neno hilo kabla. Kwa kweli, GOAT (Mbuzi) ni mnyama mwenye pembe na ndevu. Lakini kwa Kiingereza, tunaposema mtu ni GOAT, tunamaanisha yeye ndiye Greatest Of All Time (Mchezaji Bora wa Wakati Wote), bora zaidi katika kile anachofanya.

Leo, utasikia neno hilo likitumiwa katika hali zote.

Tunapozungumzia wanariadha bora zaidi kuwahi kutokea:

  • Si amini unadhani Ronaldo ni bora zaidi. Messi alishinda Kombe la Dunia! Ni wazi yeye ndiye GOAT wa soka.

Unaweza tumia neno hilo pia kwa mtu aliyefanya kitu vizuri sana, kwa mfano kazini:

  • Bosi wangu aliniruhusu nichelewe kazini kwa saa moja leo - yeye ni GOAT.

Neno hili pia linafaa unapo mpongeza mtu aliyekusaidia:

  • Asante kwa kurekebisha kompyuta yangu. Wewe ni GOAT.

Litumie kama kivumishi, kusema kitu ni kizuri sana au cha kushangaza: 

  • Hii pizza ni goated! Lazima turudi wiki ijayo!

Linaweza kuwa muhimu pia kama unacheza michezo ya video: 

  • Mchezo huu ni goated sana.

Chunguza mfululizo mzima wa Words we use kwa kubofya hapa kusikiliza!


Credits 

Host: Gode Migerano

Written by: Nick Pagano

Graphic design: Dory Wang

Educational consultant: Professor Lynda Yates

Produced by: Dory Wang


Latest podcast episodes

Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Stream now