Ila upinzani unawasiwasi kuwa mfuko wa matumizi wa serikali, ni ukarabati wa haraka tu usio na busara.
Na kwa waustralia wakongwe, bajeti hii inahusu kupunguza umri, wa wakati mapato ya mauzo ya nyumba yanaweza tumiwa, kupiga jeki hela zakustaafu. Kuna taarifa kuwa kuanzia Julai mwaka ujao wa 2022, watu wenye umri wa miaka 60 na zaidi, wataruhusiwa kutumia baadhi ya faida zao za mauzo wakati umri wa sasa ni miaka 65 na zaidi.
Mweka hazina wa taifa Josh Frydenberg amesema, mabadiliko ni muhimu kwa sababu itawapa wastaafu uhuru zaidi.Hotuba ya bajeti ya mweka hazina, inatarajiwa kuanza usiku wa Jumanne, mida ya saa moja unusu kwa masaa ya mashariki Australia.