Hali hiyo imejiri wakati jimbo la New South Wales limeshuhudia ongezeko kubwa zaidi la COVID-19 mwaka huu, jimbo hilo likiwa chini ya vizuizi kwa wiki nyingine moja.
Kufikia wakati tulikuwa tukiandaa makala haya, kuna kesi 47 ambazo zimethibitishwa jimboni Qld. Wakati huo huo, hakuna kesi yoyote mpya ambayo imerekodiwa katika jimbo la magharibi Australia, wakati mji wa Perth na kanda ya Peel zinaondoka kutoka makatazo ya siku 4.
Zaidi ya idadi ya watu milioni mbili mjini Perth na kanda ya Peel, walijeshewa baadhi ya uhuru wao, jana jumamosi baada ya makatazo ya siku nne kuisha usiku wakuamkia. Hakuna kesi mpya ndani ya jamii iliyo rekodiwa katika jimbo hilo, hatakama bado jimbo hilo lina kesi nne ndani ya karantini ya hoteli.
Vizuizi vya muda vitatekelezwa kwa siku tatu zijazo, zikijumuisha uvaaji wa barakoa ndani na nje yamajengo, na vikwazo kwa idadi ya watu ndani migahawa.
Mtu yeyote anaye safiri nje ya mji wa Perth na kanda ya Peel, lazima avae barakoa na hataruhusiwa kulia ndani ya baa, migahawa nama hoteli.