Wanachama wa shirika hilo hushiriki katika miradi mbalimbali yakijamii, pamoja na miradi mingine ya elimu inayo andaliwa nakusimamiwa na viongozi wa shirika hilo.
Pascazie ndiye kiongozi wa shirika hilo, katika mazungumzo maalum na Idhaa ya Kiswahili ya SBS aliweka wazi baadhi ya kazi ya shirika lake, na alizungumzia pia tukio maalum ambalo yeye pamoja na viongozi wenza wana andalia wanachama wao kuadhimisha siku yawanawake iliyokuwa tarehe 8 Machi.
Tukio hilo litakuwa katika ukumbi wa Auburn Community Centre, 44a Macquarie Road, Auburn, NSW, Australia kuanzia saa nane za mchama Jumamosi 18 Machi. Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.