Serikali ya shirikisho inaendelea kupinga wito wakitaifa, wakuingilia kati kuzuia familia yaki Tamil kufukuzwa nchini.
Waziri Mkuu Scott Morrison, ameonya hatua yoyote kama hiyo yakuingilia kati, inaweza toa motisha kwa usafirishaji haramu wa watu.
Vita vyakisheria kwa niaba ya familia hiyo, vina endelea wakati familia hiyo inazuiwa ndani ya kituo cha uhamiaji cha Christmas Island.
Mahakama ya shirikisho itasikiza kesi hiyo Jumatano kabla ya, amri inayo zuia familia hiyo kurejeshwa Sri Lanka kuisha.
Share





