Tanzania imetoa onyo kali kwa wale wanaotoa na kusambaza taarifa za magonjwa ya mlipuko ikiwemo janga la Corona.
Onyo hilo linatolewa wakati madhehebu ya dini yakieleza hali ilivyo katika taasisi zao kuhusiana na janga hilo ambalo linaendelea kuisumbua dunia. Msemaji Mkuu wa serikali Hassan Abbas amesema ni kinyume cha taratibu mtu kutoa taarifa zinazohusiana na majanga kama vile mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona.
Rais wa Sudan Kusini ameamuru kusitishwa kwa huduma za moja ya kampuni za ndege nchini humo, baada yake kuanguka siku ya jumanne nakuwauwa abiria wote. Miongoni mwa waliofariki, ni rubani kutoka Kenya, rubani mwenza kutoka Sudan Kusini na abiria saba wakike.