Hata hivyo, vyama vya upinzani vimesema matokeo hayo niya udanganyifu. Wakati huo huo Jumapili Bw Wine, alituma ujumbe kwa mtandao wa twitter kuwa vikosi vyakijeshi, havikuwa vikimruhusu yeye na mkewe Barbie, kuondoka nyumbani, na hata kuvuna vyakula kutoka shamba lao.
Kwa upande wayo tume ya uchaguzi imesema kuwa Rais Museveni, alipokea 58% ya kura wakati Bobi Wine alipokea 38% ya kura na 52% yawaganda walipa kura kura.
Hata kama rais Museveni alibaki madarakani, angalau wanachama tisa wa baraza lake lamawaziri, naibu rais akijumuishwa, walishindwa katika uchaguzi huo, wengi wao wakishindwa katika uchaguzi huo na wagombea wa chama cha Bw Wine.