Ila katika sherehe ya tuzo hizo ya mwaka huu wa 2021, historia ilitengenezwa baada ya wanawake wanne kunyakua tuzo hizo katika vitengo vyote.
Rosemary Kariuki ni mmoja wa wanawake husika walio tengeza historia katika sherehe za tuzo hizo. Katika mazungumzo maalum na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, Bi Rosemary aliweka wazi hisia zake kuhusu tukio hilo lakihistoria pamoja na majukumu mapya ambayo ame rithi kupitia ushindi wake.