Licha ya changamoto anazo kabili, Bi Rosemary anasababu nyingi yakurufahi nakusherehekea katika mwanzo wa mwaka huu.
Mwaka wa 2021 umeanza vizuri sana kwa Bi Rosemary Kariuki, mwanzo kabisa alitangazwa mshindi wa tuzo ya Shujaa wa jamii ya Australia katika jimbo la New South Wales, na wiki chache baadae Waziri Mkuu wa Australia, alimtangaza Bi Rosemary kuwa ni mshindi wa tuzo hiyo pia kitaifa mjini Canberra.
Katika mazungumzo maalum na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, Bi Rosemary Kariuki aliweka wazi hisia zake kuhusu kushinda tuzo hiyo. Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.