Katika utafiti wa hivi karibuni wa waomba hifadhi na wakimbizi wa LGBTQIA+, mazingira yaki asili hayakutumika tu kama mahali pa kukutania, bali kama mazingira ambapo washiriki walihisi salama bila kuhojiwa au kuhukumiwa.
Ian Seal ni mkurugenzi mtendaji wa Many Coloured Sky, shirika linalowasaidia wakimbizi na waomba hifadhi wa LGBTQIA+ mjini Melbourne. Aliiambia SBS Examines kwamba upweke ni tatizo kubwa katika jamii.
"Watu kutoka asili yao ya kitamaduni ndio ambao wanahisi hawana usalama nao na hawahusiani nao sana hapa Australia, kwa sababu wanawakilisha utamaduni ambao watu wamelazimika kuukimbia," alisema.
"Wanachama wengi wa jamii yetu wanazungumzia kuhusu kulazimika kufanya uchaguzi kati ya: Je, nitaendelea kuhusishwa na utamaduni wangu na historia yangu, familia yangu na jamii yangu? Au nitapata nafasi katika jamii ya LGBTIQ+?"
Mim alilazimika kufanya hivyo baada ya kuhamia Australia kutoka Vietnam miaka 11 iliyopita.
"Nilikuwa na haya sana na Kiingereza changu kilikuwa kidogo. Kwa hivyo nilikaa zaidi na jamii yangu ya Kivietinamu. Nilificha ujinsia wangu na utambulisho wangu pia," waliambia SBS Examines.
Mim alialikwa kushiriki katika programu ya wiki nane inayozingatia mazingira pamoja na wakimbizi wengine 36 wa LGBTQIA+ na wanaotafuta hifadhi.
Washiriki walitazama ndege, walichanjia milo na kutafakari nje, walitembea kando ya ufuo, na walitunza bustani
Mtafiti mkuu Nerkez Opacin aliiambia SBS Examines kwamba kufuatia programu hiyo, kulikuwa na kupungua kwa upweke wa washiriki, na ongezeko la uhusiano wao na mazingira yaki asili.
"[Mazingira yaki Asili] hutumika kama msingi usioegemea upande wowote, usiohukumu wa kuunganisha."
Mim alisema kwamba programu hiyo ilikuwa njia laini kwao kukutana na watu na kuungana.
"Mazingira yaki Asili yanaponya ... nahisi amani."
Katika makala haya ya SBS Examines, tunachunguza jinsi mazingira yaki asili yanaweza saidia kukabili upweke.





