Vikao vya Tume ya Kifalme kwa Unyanyasaji wa Wayahudi na Uwiano wa Kijamii vimefichua kwamba waathiriwa na wahusika wengi wa chuki dhidi ya Wayahudi nchini Australia ni watoto. Tunawezaje kujadili suala hilo kwa njia inayofaa umri wa watu?
Mwanasaikolojia wa kimatibabu Amanda Gordon, aliambia SBS Examines, kumekuwa na idadi inayoongezeka ya familia zinazo wasiliana naye zikiomba ushauri kuhusu jinsi yakuzungumza na watoto wao kuhusu chuki dhidi ya Wayahudi.
Watoto wanakuja na maswali kama, kwa nini watu wanawachukia Wayahudi? Je, tuko salama? Kwa nini kuna walinzi shuleni kwetu?
Amesema watoto wa umri tofauti, wanahitaji majibu tofauti.
Olga Weintraub Elia ni mwalimu wa elimu ya mapema ya watoto, amesema hata watoto wadogo wanaweza elewa umuhimu wa wema na utofauti.
"Silazima utoe maelezo yakisiasa ila, unaweza zungumza kuhusu haki, kuwa mkarimu, na heshima," alisema.
Shoshana, ni mwalimu wa wanafunzi wa shule ya sekondari, amesema inaweza kuwa vigumu kupitia mazungumzo haya na vijana.
Si kama wame ona chuki dhidi ya Wahayudhi, ni wakati wame ona chuki dhidi ya Wayahudi.
Shoshana amesema wanafunzi wake mara nyingi huchangia utani au meme mtandaoni, bila kujua zina mizizi ya chuki dhidi ya Wayahudi.
"Unastahili zungumza nao kuihusu, kwa ukweli... waonyeshe mawazo ya busara yanaonekanaje linapokuja suala la mambo kama chuki dhidi ya Wayahudi na ubaguzi wa rangi."
Katika makala ya wiki hii, SBS Examines ina uliza — tunastahili zungumzaje na watoto kuhusu chuki dhidi ya Wayahudi?
Wasikilizaji wanaotafuta msaada wa dharura wanaweza wasiliana na Lifeline kwa: 13 11 14, na unaweza piga simu kwa kupata msaada kwa Watoto kwenye namba hii: 1800 55 1800 kwa vijana wenye umri wa hadi miaka 25.






