Mwongozo wa Makazi: Jinsi ya kutuma fedha nje ya nchi

Dola za Australia zatumiwa katika biashara duniani

Dola za Australia zatumiwa katika biashara duniani Source: Getty Images

Kote duniani, watu zaidi ya milioni 250 wanaishi nje ya nchi yao ya kuzaliwa na wahamiaji wengi huchagua kutuma fedha kwa familia nyumbani.


Waustralia pia wanahamisha fedha zaidi nje ya nchi kuliko hapo awali, lakini gharama za siri zinaweza kuwa kubwa sana. Wakala mbalimbali wa utumaji pesa wana kikomo cha kiwango tofauti cha kiasi cha fedha ambazo huwaruhusu wateja kutuma nje ya nchi.

Hata hivyo, chini ya sheria ya Shirikisho la sasa, taasisi zote za fedha za Australia zinahitajika kutoa taarifa za fedha kwa kiwango cha $10,000 au zaidi kwa mdhibiti AUSTRAC, ikiwa ni pamoja na maelezo ya wamiliki wa akaunti husika.

Taarifa za Akaunti za Australia na Kituo cha Uchumbuzi husimamia shughuli za kifedha ili kutambua matukio ya ubatilishaji fedha chafu, uhalifu uliopangwa na ukwepaji wa kodi.


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service