Mawaziri husika wamekana shutma zote dhidi yao, hata hivyo mawaziri hao wanaendelea kukabiliwa kwa changamoto kutoka kwa vyama vya upinzani na wadau wengine katika jamii.
Otieno Makoochieng ni mtaalam wa maswala yakisiasa na sheria nchini Australia. Katika mazungumzo maalum na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, Bw Otieno aliweka wazi changamoto zakisheria, zinazo wakabili mawaziri husika na kama serikali iko sahihi kusema uchunguzi huru, hau hitajiki kwa maswala hayo.