Waheshimiwa wa Australia wame sherehekea maisha ya Prince Philip mume wa malkia wa Uingereza katika ibada ndani ya kanisa mjini Sydney. The Duke of Edinburgh alifariki usingizini Ijumaa tarehe 9 Aprili, miezi mbili kabla ya siku yake yakuzaliwa ambapo angefikisha miaka 100.
Uchunguzi kwa kifo cha msichana mwenye miaka saba katika hospitali ya Perth, utachunguza kama upendeleo wa tamaduni, au vizuizi vya lugha vilisababisha maombi ya wazazi wake kupuuzwa. Huduma ya afya ya watoto na vijana ya Magharibi Australia, imesema itachunguza kama tamaduni ya familia hiyo ilishawishi huduma waliyo pokea.
Rais Samia Suluhu Hassan ameenda nchini Uganda hii leo kwa ziara ya kikazi ya siku moja kufuatia mwaliko aliopewa na Rais Yoweri Museveni wa nchi hiyo. Rais Samia pamoja na mwenyeji wake Rais Museveni, watahudhuria hafla na kushuhudia utiaji saini wa mkataba kati ya Serikali ya Uganda na Kampuni ya Mafuta Ghafi ya Afrika Mashariki (EACOP) juu ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la kutoka Hoima nchini Uganda kwenda Tanga nchini Tanzania.