Jimbo la Queensland limerekodi kifo cha saba cha COVID-19, tangu mwanzo wa janga hili. Afisa mkuu wa matibabu Jeannette Young amesema mwanaume huyo alikuwa na umri wa miaka themanini na, alikuwa muAustralia aliyerejea nyumbani kutoka Philippines nakupitia Papua New Guinea. Kifo hicho kimejiri wakati, kesi mbili mpya za COVID-19, zimerekodiwa ndani ya karantini ya hoteli.
Kiongozi wa jimbo la Magharibi Australia amejiunga na mamlaka ya huduma ya dharura, kuchunguza uharibifu uliosababishwa na kimbunga Seroja katika eneo la pwani yakati ya magharibi ya jimbo hilo. Alipotembelea mji wakitalii wa Kalbarri ulio athiriwa, ambako 70% ya mali iliharibika, Mark McGowan amesema ni ajabu hakuna mtu aliye uawa wakati upepo wenye kasi ya kilomita 170, iligonga usiku wa Jumapili.
Kanisa Katoliki nchini Kenya linaitaka serikali kusimamisha mpango wake wa kufunga kambi za wakimbizi za Dadaab na Kakuma na kuendelea kuwapa hifadhi wakimbizi hao. Kanisa limesema wakimbizi hao zaidi ya 500,000 kutoka mataifa 15 wanaoishi nchini humo, itakuwa ni hatari kubwa kwa usalama wao endapo watarejea katika mataifa yao. Ombi hili linatolewa siku chache baada ya mahakama nchini humo kusitisha utekelezaji wa agizo la serikali ya Rais Uhuru Kenyatta kutaka kuzifunga kambi hizo hadi kesi iliyowasilishwa mahakamani isikilizwe na kutolewa maamuzi.