Waziri Mkuu Scott Morrison amekosolewa kwakusema kuwa, maandamano yahaki yajumatatu, yalikuwa ushindi kwa sababu waandamanaji hawaku kabiliwa kwa risasi. Kiogozi wa chama cha Greens Adam Bandt pamoja na seneta Larissa Waters, wanataka awaombe msamaha wanawake walio andamana, wakisema kuwa kauli yake ni tusi kwenye ujumbe.
Serikali ya Marekani Jumatatu imetoa msaada wa dola za Kimarekani Milioni 8 kwa ajili ya wakimbizi wanaoishi kwenye baadhi ya kambi nchini Tanzania, huku kukitolewa wito kwa wakimbizi ambao nchi zao sasa zina amani kurejea makwao kwa hiari. Msaada huo wa fedha utakaosaidia chakula kwa wakimbizi waliopo katika kambi za Nduta, Mtendeli na Nyarugusu Kaskazini Magharibi mwa Tanzania, umetolewa na Marekani mjini Dar es Salaam kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa,USAID, kwa Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa, WFP, kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania.
Jumuiya ya kimataifa imetoa wito wa utulivu na kujizuia baada ya waandamanaji wapatao 20 kuuliwa Jumatatu (15.03.2021) katika maandamano ya kupinga mapinduzi ya kijeshi Myanmar. Shirika linalofuatilia matukio ya mauaji na watu kukamatwa Myanmarlimesema watu wasiopungua 20 waliuwawa siku ya Jumatatu, kufuatia machafuko na maandamano dhidi ya utawala wa kijeshi, wiki sita tangu jeshi lilipotwaa madaraka.