Serikali ya shirikisho ime saini mkataba wenye thamani ya dola bilioni 1.8, na jimbo la Kusini Australia, kwa ajili yakupunguza bei ya umeme nakuboresha utoaji wa nishati yakutegemewa. Kama sehemu ya mkataba huo, vifaa vya gesi vitafunguliwa na kazi itaanza kwa kiunganishi kipya kati ya majimbo ya Kusini Australia na New South Wales.
Baadhi ya viongozi katika kikao cha 75 cha mkutano wa 59 wa Umoja wa Mataifa (UN) uliofanyika siku ya Ijumaa Aprili tarehe 16, 2021 wametambua alama za uongozi za za aliyekuwa rais wa Tanzania, Hayati John Magufuli. Viongozi hao wameahidi kuendelea kushirikiana na rais wa sasa wa taifa hilo Samia Suluhu Hassan .
Maelfu ya waendesha magari na wasafiri walijipata mashakani usiku wa Jumamosi baada maafisa wa usalama jijini Nairobi kufanya oparesheni ya kuhakikisha wakazi wa jiji wanazingatia sheria ya kutotoka nje kuanzia saa mbili usiku hadi saa kumi afajiri. Hakuna magari yaliyoruhusiwa kuingia au kutoka katika mji mkuu. Katika baadhi ya barabara polisi waliwaagiza waendesha magari kuzima injini, kutoka ndani ya gari na kukaa kando ya barabara.