Taarifa ya Habari - 19 Juni 2022

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Serikali ya New South Wales inawasilisha mfumo wa nyumba wenye thamani ya $780.4 milioni, kwa wanao nunua nyumba kwa mara ya kwanza.


Wataalam wa afya nchini Australia wanasema taifa inastahili zingatia kufuata mfano wa Marekani kutoa chanjo kwa watoto ambao wana chini ya miaka mitano dhidi ya UVIKO-19. Hatua hiyo imejiri baada ya mamlaka ya vyakula na madawa ya marekani, kuidhinisha chanjo mbili za Moderna na Pfizer kwa watoto wenye chini ya miaka mitano.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inataka Rwanda izuiliwe kushiriki katika kuundwa kwa kikosi cha kijeshi, cha kikanda, kilichopendekezwa, katika juhudi za kuimarisha usalama nchini humo. Serikali ya Rais Felix Tshisekedi inaiomba Uingereza kuishinikiza Kigali kukomesha kile ilichokiita "uchokozi" wake, Kinshasa imesema. Huu ni mzozo wa hivi punde kati ya majirani hao wawili, ambao wana historia ya miongo kadhaa ya malumbano, na hivi karibuni kumeshuhudiwa mapigano ya hapa na pale kwenye mpaka wao wa pamoja.

Watetezi wa haki za kiraia na mawakili wa jamii ya wamaasai, wanaendelea kuishinkiza serikali ya Tanzania kuachana na mpango wa kuwafurusha maelfu ya wamaasai ambao ni wafugaji wa kuhama hama, kutoka kwenye ardhi yao ya asili mashariki mwa mbuga ya kitaifa ya Serengeti. Sehemu hiyo ndiyo njia wanayotumia wanyama wakati wa msimu wa kuhama hama. Makabiliano hayo ya JunI tarehe 10 yalitokea Loliondo, ambayo ni sehemu ya hifadhi ya Ngorongoro.


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service