Jeshi la Myanmar hii leo limetwaa madaraka katika mapinduzi ambayo hayakuwa ya umwagaji damu, na kumshikilia kiongozi wake aliyechaguliwa kwa njia ya demokrasia Aung San Suu Kyi na kutangaza hali ya hatari ya mwaka mmoja.
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Bobi Wine amewasilisha changamoto ya kisheria kwa mahakama ya juu nchini humo akiomba kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa rais wa mwezi Januari ambayo yalimpa ushindi rais wa muda mrefu Yoweri Museveni. Bobi Wine ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi mwenye umri wa miaka 38 ameyapinga matokeo hayo na kusema anaamini kwamba ushindi wake uliibiwa.
Wizara ya Afya nchini Tanzania imesema Jumatatu haina mpango wa kupokea chanjo ya COVID-19 ambayo imekuwa ikiripotiwa kuwepo na kutumika katika mataifa mengine. Akiwa katika ofisi za wizara mjini Dodoma, Dkt Gwajima amesema dhumuni la ufafanuzi huo ni juu ya maswali kadhaa ambayo amekuwa akiyapokea kutoka kwa wanahabari kuhusu kujikinga na magonjwa ya kuambukiza na yasiyo kuwa ya kuambukiza.