Shirika lakitaifa linalo wakilisha wanao toa huduma za uzeeni katika makazi yawazee, nyumbani nakatika makazi ya ustaafu, limesema linatumai serikali ya shirikisho inachukua fursa yakubadili kabisa sekta hiyo. Tume yakifalme kwa huduma ya uzeeni imetoa mapendekezo 148 kwa hatma ya usoni ya sekta hiyo, ikijumuisha sheria mpya ya huduma ya uzeeni, inayo weka haki zawazee nakutoa haki ya wote kwa huduma ya hali ya juu.
Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu baada ya kukutwa na hatia ya ufisadi na kueneza ushawishi. Hukumu hiyo iliyotolewa leo na mahakama mjini Paris inajumuisha mwaka mmoja gerezani na miaka miwili ya kifungo cha nje. Baadae mwezi huu, Sarkozy atakabiliwa na kesi nyingine pamoja na watu wengine 13 kwa mashtaka ya kufadhili kinyume cha sheria kampeni yake ya urais mwaka 2012.
Ripoti ya ndani ya serikali ya Marekani ambayo gazeti la The New York Times imeipata inasema kuwa Ethiopia inaendesha “kampeni maalum ya kutokomeza kabila moja”. Kampeni hiyo inafanyika kwa kisingizio cha vita katika mkoa wa Tigray, eneo ambalo kwa kiasi kikubwa linadhibitiwa na wanamgambo wa Amhara upande wa kaskazini mwa nchi.