Bajeti ya Mei kujumisha mfuko wa dola bilioni 1.7, kwa huduma yamalezi yawatoto, kwa ajili yakuwaruhusu wazazi wengi zaidi warejee kazini. Hata hivyo kiongozi wa upinzani Anthony Albanese, amesema Scott Morrison amekosa fursa yaku karabati matatizo ambayo, sera yake nyenyewe ya huduma ya malezi ya watoto ili unda.
Duru ya tatu ya mazungumzo na Iran juu mpango wake wa nyuklia yaliyokuwa yanafanyika mjini Vienna, Austria yameahirishwa. Wajumbe wa Ulaya waelezea wasiwasi wao juu ya kujikongoja kwa mazungumzo hayo.
Kiongozi mashuhuri wa genge lililojihusisha na vitendo vya utekaji nyara wa wanafunzi zaidi ya 300 nchini Nigeria mnamo Desemba ameuawa na genge hasimu, maafisa wanasema.