Siku moja baada ya kuanza tena kwa safari kati ya Australia na New Zealand, mfanyakazi katika uwanja wa ndege wa Auckland amepatwa na virusi vya COVID-19. Mamlaka wa afya ya New Zealand wamesema mtu huyo, anajitenga nyumbani na juhudi zakutafuta alio kutana nao zinaendelea.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta anatarajiwa wiki hii kuunda jopo la uteuzi la makamishna wanne wa Tume ya Uchaguzi, IEBC, kujaza nafasi za makamishna wanne waliojiuzulu baada ya uchaguzi mkuu wa 2017. Tume ya uchaguzi (IEBC) hivi sasa ina makamishna watatu pekee. Ripoti ya BBI inapendekeza haja ya kuwa na makamishna wapya kwa tume hiyo kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022.
Rais Xi Jinping wa China amesema mfumo wa utawala wa kilimwengu lazima ufanywe uwe wa usawa na uadilifu zaidi, na kwamba kanuni zinazowekwa na nchi moja ama baadhi ya mataifa haziwezi kulazimishwa kufuatwa na wengine.