Taarifa ya Habari 20 Juni 2021

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Chanjo ya Covid-19 inayo undwa jimboni Victoria, itakuwa ya kwanza nchini Australia, kutumia teknolojia ya mRNA kufika hatua ya kwanza yamajaribio ya zahanati.


Taasisi ya Monash Institute of Pharmaceutical Sciences, itatengeza dozi za chanjo kwa majaribio ambayo, inatarajiwa kuanza baadae mwaka huu. Serikali ya Victoria imetangaza uwekezaji wa dola milioni tano kutoka kwa mfuk owa dola milioni hamsini, kutengeza uwezo wa uzalishaji wa mRNA jimboni humo.

Mamlaka wa afya jimboni New South Wales wana hamasisha wakaaji waka fanye vipimo vya COVID-19, baada yakutambua kesi zingine mpya wikendi hii.Mlipuko katika vitongoji vya mashariki Sydney, umeongezeka kwa maambukizi tisa hii leo jumapili 20 Juni, wakati vizuizi vinawekwa katika maeneo kadhaa ya mji huo. Kwa sasa ni lazima kuvaa barakoa ndani ya majengo yote yamatukio, katika vitongoji vyote saba vinavyo jumuisha Waverley, Woollahra, Randwick, Bayside, Canada Bay, Inner west, na C-B-D.

Waendesha mashtaka nchini Rwanda Alhamisi wameiomba mahakama ya juu nchini humo kumhukumu kifungo cha maisha jela mkosoaji mkuu wa serikali ya Rwanda, Paul Rusesabagina, kwa tuhuma za ugaidi. Rusesabagina hakuwepo mahakamani wakati wa kusikilizwa kesi dhidi yake na watuhumiwa wenzake 21. Amekuwa akisusia kufika mahakamani akidai kwamba mahakama za Rwanda hazina mamlaka ya kumfuatilia kwa sababu ya uraia wake wa Ubelgiji, na kueleza kuwa mfumo wa sheria wa nchi hiyo hauwezi kumtendea haki kwa sababu hauko huru. Mahakama inatarajiwa kutoa maumuzi yake katika muda usiozidi siku 90.

 


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service