Waziri mkuu Scott Morrison amesema anataka uchunguzi unao fanywa, kwa jibu la shutma la ubakaji wa mfanyakazi wa zamani wa chama cha Liberal, ulete mageuzi ya muda mrefu yakitamaduni.
Rais wa Marekani Joe Biden ameanza msukumo wa kidiplomasia kufufua mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 kati ya Iran na mataifa yenye nguvu duniani. Wanaounga mkono makubaliano hayo wanasema atahitaji juhudi za muda mrefu kufanikisha, wakati wapinzani wanasema ajikite badala ya kuishinikiza Tehran kuingia makubaliano mapya na mazito zaidi.
Maafisa 27 wa Ikulu ya Sudan Kusini wamethibitihswa kuwa wameambukizwa virusi vya corona na kwa sasa wamewekwa karantini. Ateny Wek Ateny,ambaye ni msemaji wa Rais Salva Kiir, aliliambia shirika la habari la Ujerumani DPA kwamba walioambukizwa wanatumikia katika idara za ulinzi, huduma za mapishi na udereva, pamoja yeye mwenyewe msemaji wa rais.