Gwiji wa mtandao wakijamii Facebook, inatishiwa kwa hatua zakisheria na shirika la haki zawa Islamu la Australia. Shirika la The Australian Muslim Advocacy Network au, shirika la Mtandao wa utetezi wa Waislamu wa Australia linalo julikana kwa ufupi kama [[AMAN]], limedai kuwa Facebook imeruhusu ubaguzi dhidi yawaislamu kuendelea mtandaoni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Samia Suluhu Hassan, Jumamosi ameongoza viongozi na wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam kuuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.
Maafisa wa usalama wa jimbo la Georgia Marekani wamesema wamemkamata mwanaume mmoja anayeshukiwa kuwapiga risasi na kuwaua watu wanane, sita kati yao wakiwa ni wanawake wa asili ya Asia.