Taarifa ya Habari 22 Juni 2021

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Wakaaji wote wa Sydney kuvaa barakoa kwa wiki ya ziada katika sehemu za ndani zamatukio, baada ya ongezeko la visa vya maambukizi ya COVID-19 ndani ya jamii.


Mfanyakazi katika ndege aliye ambukizwa COVID-19 alipokuwa ndani ya karantini hotelini, amemuambukiza mwanaume mmoja katika sehemu ya tukio ambako watu 30 walikuwa mjini Brisbane. Hata hivyo mamlaka jimboni Queensland wana amini hatari kwa maambukizi ndani ya jamii ni ndogo. Afisa Mkuu wa matibabu wa Queensland Dr Jeannette Young amesema, mamlaka wanajaribu kufuatilia watu wowote ambao walijumuika na mtu huyo kupitia kanda za video.

Baada yakuwa katika jangwa la kisiasa nchini Australia kwa miaka kadhaa, hatimae Barnaby Joyce ameapishwa kwa mara ya pili nakuwa naibu waziri mkuu wa taifa. Bw Joyce aliapishwa rasmi mapema hii leo, katika sherehe ndani ya nyumba ya serikali, na Gavana Mkuu David Hurley. Waziri Mkuu Scott Morrison alishiriki katika hafla hiyo, kupitia intanet na alimpongeza Bw Joyce kwa uteuzi wake.

Mwakilishi wa umoja wa Ulaya, Claude Boshu, amebainisha kuwa msaada wa euro milioni 430 uliokuwa utolewe kwa kipindi cha 2015 hadi 2020 sasa utatolewa baada ya kupokelewa kwa mazungmzo na raia Evariste Ndayishimiye. Msemaji wa rais Ndayishimiye amesema rais ameikaribisha hatua hiyo. Baada tu ya kupokelewa kwa mazungumzo na rais Evariste Ndayishimiye, mwakilishi wa Umoja wa Ulaya nchini humu Claude Boshu amesema hatua ya kusimamishwa vikwazo imechukuliwa baada ya wataalam wa halmashauri mbali mbali za umoja huo kukutana na kuangazia hali ya Burundi.


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service