Taarifa ya Habari 22 Oktoba 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Mfalme Charles na Malkia Camilla waanza sehemu ya mwisho, ya ziara yao mjini Sydney, katika sehemu ya ziara yakifalme.


Viongozi wa shule katika jimbo la New South Wales, wakubaliana kwa sauti moja na uongozi wa jimbo hilo kupiga marufuku matumizi ya simu za rununu shuleni.

Kamati ya Seneti yapokea mawasilisho kuhusu muswada mpya wa huduma ya wazee, imesikiza maoni kuwa kutoa muda wa saa moja kwa wiki kwa shughuli za usaidizi hautoshi kuwahudumia wazee ipaswavyo.

Makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyodumu kwa wiki kadhaa yamevunjika baada ya kuanza mapigano mapya katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kati ya waasi wa M23 na wanamgambo wanaoungwa mkono na serikali.

Naibu Rais aliyeondolewa mamlakani nchini Kenya Rigathi Gachagua, Jumapili alimshamblia mkuu wake William Ruto akisema ni “mbaya sana” na mkatili, akionya kuwa maisha yake yanaweza kuwa hatarini.

Watu wasiojulikana walimteka nyara, kumpiga na kumjeruhi vibaya afisa mwandamizi wa chama cha upinzani nchini Tanzania Chadema kabla ya kumtupa msituni, chama chake kilisema siku ya Jumapili, mwezi mmoja baada ya kutekwa nyara na kuuawa kwa kiongozi mwingine wa chama hicho.

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service
Taarifa ya Habari 22 Oktoba 2024 | SBS Swahili