Rais Joe Biden ameamuru bendera kupeperushwa nusu mlingoti, baada ya idadi ya vifo vya wa Marekani kutokana na Covid-19 kupindukia 500,000. Biden ameonya idadi hiyo huenda ikaongezeka kama hatua zaidi hazitachukuliwa.
Rais Sergio Mattarella wa Italia amelaani mauaji dhidi ya balozi wa nchi yake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Luca Attanasio. Balozi huyo ameuawa mchana wa leo wakati msafara wa Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa, WFP, ulipovamiwa na watu wenye silaha mashariki mwa Kongo.
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine amesema mapema Jumatatu amefuta kesi aliyowasilisha mahakamani kupinga ushindi wa Rais Yoweri Museveni kwenye uchaguzi wa Januari kwa madai kuwa mahakama ya juu inaegemea upande mmoja. Kwa mujibu wa shirika la habari la Uingereza, Reuters, Bobi Wine ameyasema hayo wakati akiongea na wanahabari mjini Kampala.