Wanao toa huduma ya wazee wanaomba hatua za haraka, wakati UVIKO-19 ina athiri zaidi ya theluthi tatu ya vifaa vya huduma ya wazee nchini Australia.
Shirika la Marekani la maendeleo ya kimataifa USAID limetangaza kwamba litaipatia Kenya dola milioni 255 kama msaada wa dharura na maendeleo kukabiliana na ukame uliokithiri na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amewaomba viongozi wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki kukubali maombi ya Somalia kuwa mwanachama wa jumuiya hiyo.
Peter Bol apeperusha bendera ya Australia katika fainali ya 800m ya michuano ya dunia ya riadha ya Oregon, na historia yatengezwa katika fainali ya kombe la Afrika la wanawake, wakati mataifa kadhaa yajikatia tiketi za nusu fainali ya kombe la wanawake la Ulaya.