Chama cha Australian Greens kimedokeza kuwa kina taka weka mhuri wao, kwa bunge mpya ambayo ime anza vikao vya kwanza mjini Canberra leo Jumanne 26 Julai, ikiwa na wanachama wengi zaidi wa vyama vidogo. Kiongozi wa chama cha Greens Adam Bandt, amesema watasukuma serikali isi idhinishe miradi yoyote ya mipya ya makaa ya mawe au gesi.
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov amewasili nchini Uganda katika ziara yake ya tatu katika nchi za Afrika, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Urusi ametangaza Jumatatu. Lavrov alilakiwa mjini Entebbe na mwenzake wa Uganda, Jeje Odongo, amesema Maria Zakharova akichapisha picha ya mawaziri hao wawili kwenye mtandao wa Telegram. Kwa mujibu wa shirika la habari la Urusi TASS, Lavrov anatarajiwa kufanya mazungumzo na Rais wa Uganda Yoweri Museveni leo Jumanne.
Liberia imeruhusu uraia pacha, na hivo kubatilisha marufuku ya muda mrefu iliyochukuliwa na baadhi ya watu kama ya kinafiki kwani wasomi wengi walikuwa na uraia wa Marekani kwa siri. Mswada huo ambao ulisainiwa kuwa sheria na Rais George Weah siku ya Ijumaa na kuthibitishwa na shirika la habari la AFP Jumapili, ulipitishwa na Bunge na baraza la Seneti siku ya Jumanne. Raia wenye urai pacha hata hivyo, hawataruhusiwa kuhudumu kama rais, waziri wa fedha na mkuu wa benki kuu au kushikilia nyadhifa muhimu katika vyombo vya usalama wa taifa na sheria.