Uingereza imechapisha maelezo ya makubaliano yake finyu ya biashara na Umoja wa ulaya, siku tano tu kabla ya kutoka katika moja ya umoja mkubwa zaidi wa kibiashara Duniani, katika mabadiliko yake makubwa ulimwenguni, tangu kupotea kwa himaya.
Walinda amani watatu wa Umoja wa Mataifa kutoka Burundi wameuawa na wengine wawili wamejeruhiwa katika kile UN imekiita “shambulizi lililofanywa na wapiganaji wenye silaha wasiojulikana” Ijumaa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati wakati nchi hiyo ikielekea katika uchaguzi mkuu Jumapili.
Uganda imesitisha kampeni zote za uchaguzi wa urais katika mji mkuu wa Kampala na wilaya nyingine 10 zenye idadi kubwa ya watu. Msemaji wa Tume ya Uchaguzi, Paul Bukenya, amesema sababu ya kufuta kampeni ni ongezeko la maambukizo ya virusi vya corona.