Taarifa ya Habari 27 Machi 2025

Bench - Swahili.jpg

Msemaji wa maswala ya hazina katika Upinzani amethibitisha kuwa Upinzani wa Mseto, utafuta makato ya ushuru ya Labor, upinzani ukishinda uchaguzi mkuu.


Mwanasheria mkuu wa New South Wales amesema jeshi la polisi halina uhakika kilicho fanywa na faili elfu 9 zilizo pakuliwa kutoka tovuti ya serikali katika tukio kubwa la kuvujwa kwa data. Taarifa ya polisi imesema faili hizo zilichukuliwa kutoka Idara ya Jumuiya na Haki, zinajumuisha amri zakusitisha vurugu na hati za kiapo, ambazo wataalam wa sheria wana hofu inaweza waweka waathiriwa wa unyanyasaji wa nyumbani hatarini.

Utawala wa Trump umejaribu kudhibiti utata ulio ibuka kutoka kwa taarifa zilizo vuja kuwa mwandishi wa habari, ali ongezwa katika kundi la mazungumzo ya viongozi wa ngazi ya juu ya serikali katika mtandao wa mawasiliano wa Signal, ambako maswala kuhusu mipango ya mashambulizi dhidi ya wapiganaji waki Houthi yali changiwa. Jarida la The Atlantic lime chapisha baadhi ya mawasiliano  yaliyo changiwa katika mtandao wa Signal baada ya taarifa kuvuja kuwa mhariri wa jarida hilo alikuwa ame ongezwa katika kundi hilo.

Makamu wa kwanza wa rais wa Sudan Kusini Riek Machar, mpinzani wa muda mrefu wa Rais Salva Kiir, amekamatwa jana Jumatano, hatua iliyoelezwa na Umoja wa Mataifa kuwa inaiweka nchi hiyo katika ukingo wa mzozo mpana zaidi.

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service
Taarifa ya Habari 27 Machi 2025 | SBS Swahili