Shirika la Gender Equity Victoria, ambalo hushughulikia maswala ya usawa wa jinsia jimboni Victoria, limesema uamuzi wa atakaye ongoza uchunguzi huru kwa tamaduni ya kazi ndani ya bunge, ni muhimu kwa uhalali wa uchunguzi huo. Uchunguzi huo umesababishwa na madai ya Brittany Higgins, kuwa alibakwa na mfanyakazi mwenzake ndani ya ofisi bungeni katika mwaka wa 2019, alipokuwa ame ajiriwa katika ofisi ya waziri wa ulinzi Linda Reynold.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia ameuomba Umoja wa Mataifa kufanya uchunguzi kuhusiana na mauaji ya balozi wake nchini DRC katika shambulizi la kushtukiza. Mwana Diplomasia Luca Attanasio, mwenye umri wa miaka 43, aliuwawa siku mbili zilizopita baada ya msAfara wa magari ya Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, kushambuliwa mashariki mwa nchi karibu na mpaka wa Rwanda.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Jumamosi alikabidhiwa uenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Afrika Mashariki (EAC) na mwenyekiti anayeondoka, Rais wa Rwanda, Paul Kagame. Hii ni kufuatia mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao uliohudhuriwa na viongozi wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo.