Chama hicho kiomeongezea kuwa walimu wana wasiwasi kuhusu kuanza kwa oparesheni za shule, tarehe 16 agosti, wakati kesi za COVID-19 zina endelea kuongezeka.
Afisa mkuu wa Afya wa Victoria Brett Sutton amesema wanao tafuta watu wa karibu wenye maambukizi ya COVID-19, wanafanya kazi kwa bidii kuwatambua watu wa karibu wa kesi mpya za COVID-19 jimboni humo. Jimbo hilo lilirekodi kesi mpya nne ndani ya jamii, zote zikiungwa na milipuko ya sasa, na zilikuwa zikijitenga wakati zilikuwa katika hali ambukizi. Jimbo la Victoria limepiga marufuku usafiri usio wa lazima kwa wakaaji wanao ishi katika mipaka ya jimbo hilo kuanzia saa tano na dakika hamsini na tisa za usiku wa jumanne, kwa sababu ya tisho a mlipuko wa aina ya virusi vya Delta kutoka Sydney.
Naibu wa rais wa Kenya William Ruto amezeuiwa kufanya ziara ya kibinafsi katika taifa jirani la Uganda. Vyombo vya Habari nchini humo vinaripoti kuwa Ruto alizuiwa kuabiri ndege kwenda Uganda pamoja na washirika wake kadhaa wa kisiasa. Katibu wake wa Habari David Mugonyi amesema jambo hilo ni geni kwani kwa miaka yote ambayo amehudumu kama naibu wa rais ,Ruto hajawahi kuhitaji idhini ya kusafiri nje ya nchi kutoka kwa mkuu wa utumishi wa umma.